dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, September 19, 2014

Buriani Marehemu Khamis Ali Khamis Innaa Llilaahi wainnaa Ilayhi raajiuun

**********ZANZIBAR DIASPORA**********

        Mkurugenzi Idara ya Diaspora Z’bar afariki 
                  Marehemu Khamis Ali Khamis 

Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora katika serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Khamis Ali Khamis (pichani), amefariki dunia ghafla akiwa na umri wa miaka 52.

Alifariki nyumbani kwake Mkele usiku wa kuamkia jana baada ya kuugua ghafla ugonjwa wa shinikizo la damu.
Juzi marehemu alishiriki hafla ya kumpokea Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, aliekuwa akitokea Comoro katika uwanja wa ndege wa Zanzibar.

Marehemu alianza elimu yake ya msingi mwaka 1969 na kumalizia elimu ya sekondari mwaka 1983.

Mwaka 1986 alianza masomo ya stashahada ya lugha katika Taasisi ya Kiswahili na Lugha za Kigeni (TAKILUKI) na baadae masomo shahada ya kwanza ya sayansi ya uchumi nchini Yugoslavia mwaka 1986 hadi mwaka 1993, ambako alifaulu na kutunukiwa shahada.
Mwaka 1996 hadi 1997 alifanya shahada ya uzamili ya mipango ya maendeleo vijijini nchini India.

Aidha alihudhuria masomo mafupi ya fani mbali mbali ndani na nje ya nchi kama vile ushirikiano wa kimataifa, sera kuhusiana na masuala ya uongozi, uchumi na utafiti na nyengine nyingi.

Alianza utumishi wa umma mwaka 1985 alipoajiriwa na Wizara ya Biashara, Viwanda na Utalii katika hoteli ya Bwawani akiwa mpokezi wa wageni.

Mwaka 1993 hadi 1994 alikuwa Ofisa wa Mapato katika Kamisheni ya Utalii ambapo baadae mwaka huo aliteuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Mipango katika Mamlaka ya Maeneo Huru ya Uchumi Zanzibar.

Mwaka 2007 aliteuliwa kuwa msaidizi mwandishi wa hotuba za Rais katika Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, 2008 aliteuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano na Habari Ikulu Zanzibar.

Mwaka 2011 aliteuliwa Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Ushirikiano wa Kimataifa na Wazanzibari Waliopo Nje (Diaspora) wadhifa ambao aliendelea nao hadi kufariki kwake.

Katika kipindi chote cha utumishi wake, marehemu alikuwa mchapa kazi hodari na mwenye kufanya kazi kwa ushirikiano na wenzake.

Marehemu ameacha vizuka wawili na watoto wanne, Mwenyezi Mungu ailaze pema peponi roho ya marehemu, Amiin. 


No comments :

Post a Comment